ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, May 22, 2018

ANAYEKUTANA NA BIDHAA BANDIA SOKONI SASA KUSHTAKI KWA NJIA YA SIMU.



GSENGOtV
Katika kuendelea kupambana na bidhaa bandia nchini, sasa mwananchi atawasiliana moja kwa moja kwa njia ya simu na Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA) na atapewa maelekezo ya anachotakiwa kufanya  kupata haki yake.

Hayo yamesemwa May 21 jijini Mwanza na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi Bi. Agnes Kijo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella ambaye ndiye aliyekuwa mfunguzi wa kusanyiko, wakati akiwasilisha mada katika semina ya elimu kuzijua sheria za Mamlaka hiyo kwa waandishi wa habari 

Awali ilibidi mhusika kuandika malalamiko yake na kuyatuma kwa barua pepe, au kufika ofisini jambo liliowawia vigumu watu wengi kufuatilia haki zao.

Bi. Agnes ametaja namba hiyo kuwa ni 0800 11 00 84 itakayotumika kupokea taarifa na malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara na walaji kuhusiana na changamoto wanazokabiliana nazo sokoni.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.