ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, April 22, 2018

MWANZA SIKILIZA HII YA TTCL YAANI NI ZAIDI YA DILI.



Kama ulikuwa bado hujastukia dili na michongo bomba kutoka TTCL CORPORATION, basi hii ni fursa yako kujua japo kwa uchache nikiwa na imani kwamba mwisho wa siku kali yako itakuwa "Daaaah!!! laiti kama ningelijua hili mapema ningekuwa mbali" 

Wengi wameliwa na bado wanaliwa fedha zao kupitia manunuzi ya vifurushi vya mitandao mingine isiyo ya kizalendo.

Gsengo Tv imebahatika kukutana na Meneja Masoko wa kampuni hiyo Mr. Aron Nogu, ambaye yuko katika ziara ya siku mbili mkoani Mwanza kukagua huduma za kampuni hiyo.
Askwambe mtu Aron kafunguka vyema sana juu ya huduma mbalimbali za TTCL ambazo kwa sasa zimeboreshwa na kuja na ubunifu unaoendana na mahitaji ya soko la matumizi ya sasa, ubunifu na mbinu ambazo hazipatikani katika mitandao mingine.
TTCL Corporation imechukua hatua ya kuwafuata nyumbani na mahala pa kazi wateja wake na kufanya mapinduzi makubwa ya kimawasiliano. Kupitia huduma zake mpya na zile zilizoboreshwa kama huduma ya Fiber Connect Bundle, TTCL Pesa na kadhalika, ambapo mteja  atapata huduma nne kwa pamoja zikiwa na unafuu mkubwa wa gharama na ubora wa hali ya juu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.