ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, December 13, 2017

DAWA ZA KULEVYA ZANASWA MAGU MZIGO ULIKUWA UNATOKEA TARIME.


IKITUMIA wanyama kazi yaani Mbwa, Jeshi la polisi Mkoani Mwanza linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kupatikana na dawa za kulevya katika kijiji cha Isangijo wilayani Magu mkoani Mwanza.

Watuhumiwa hao wamekamatwa wakiwa ndani ya Basi la Kampuni ya Zakaria Express linalofanya safari zake kati ya Tarime Mkoani Mara kuelekea jijini Mwanza, lenye namba za usajiri T. 813 DFV aina ya Yutong wakiwa na Dawa za kulevya aina ya Bangiiliyokuwa imehifadhiwa kwenye pakiti za nailoni ili kukwepa kukamatwa na vyombo vya dola pamoja na furushi mbili za Mirungi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.