ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, August 25, 2017

JANUARY MAKAMBA AFUNGUA KONGAMANO LA NNE LA DIASPORA ZANZIBAR




Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayeshughulikia Mazingira Mhe Januari Makamba MB) akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la nne la watanzania waishio nje ya nchi lililofanyika jana Agosti 23, 2017 Sea Cliff Hotel Mjini zanzibar

Na Mathias Canal, Zanzibar

Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) limefunguliwa jana tarehe 4 Agosti 2017 kwa kuwashirikisha washiriki wapatao 350, ambapo miongoni mwao wanadiaspora wamehudhuria zaidi ya 200 na watendaji kutoka taasisi za Serikali zote mbili wakiwa ni 150.

Diaspora wametakiwa kutumia fursa mbalimbali za uwekezaji nchini katika sekta ya kuimarisha na kuanzisha viwanda ili kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa dhamira yake ya kuifanyaTanzania kuwa nchi ya viwanda.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayeshughulikia Mazingira Mhe Januari Makamba (MB)  alipomuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia suluhu Hassan akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la nne la watanzania waishio nje ya nchi litakalodumu kwa siku mbili Agosti 23 na 24, 2017 katika ukumbi wa Sea Cliff Hotel uliopo katika kijiji cha Kama Wilaya ya Magharibi A.

Mhe Makamba alisema kuwa kwa sasa Demokrasia imeimarika nchini kutokana na serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama kukubaliana kwa kauli moja kuimarisha usalama wa wananchi ili kurahisisha uimara wa uwajibikaji wa ujenzi wa Taifa.

Alisema kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua kuwa kuna changamoto nyingi zinazowakabili Diaspora ikiwemo ucheleweshwaji wa uwekezaji sambamba na kutokuwepo sera ya utambuzi dhidi yao lakini changamoto hizo zinaendelea kutatuliwa na hatimaye kumalizika kabisa.

Changamoto zingine ilikuwa ni pamoja na kuwepo kwa uraia wa nchi mbili ambapo Mhe Makamba alisema kuwa serikali inalifanyia kazi jambo hilo kwani halipo katika uhalisia kwa sasa kwa kutokuwepo kwenye katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alisema serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi ili Diaspora waweze kutumia fursa ya uwekezaji nchini kwa urahisi huku akiwasihi kutumia fursa muhimu za uwekezaji katika Nyanja zote kwani faida itakuwa kwa Diaspora wenyewe, watanzania waishio nchini na Taifa kwa ujumla wake.

Alisema kuwa Diaspora ni kiungo muhimu katika kuchangia sehemu kubwa ya maendeleo endelevu katika nchi zao za asili kwa kuchangia katika uhamishaji wa rasilimali, ujuzi na mawazo na hatimaye kupelekea nchi yao kunufaika na uchumi wa kidunia unaoonekana kukua siku hadi siku.

Alisema kuwa fedha zinazotumiwa na Diaspora katika nchi wanazoishi ni miongoni mwa vyanzo vinavyosababisha ukuaji wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi, fedha hizo zitakapotumika vizuri kwa uwekezaji katika biashara na vitega uchumi ndio huwa chanzo na kichocheo cha ukuaji jadidifu wa pato na uchumi wa nchi zinazopokea fedha hizo.

Aidha, Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano imeweka msisitizo na juhudi za kukusanya mapato ili kukuza uchumi wa Tanzania na uwezo wa serikali kujiendesha.
Mhe Mkamba aliwasihi Diaspora kufuata kanuni,taratibu na sheria katika nchi wanazoishi ili kuendelea kuiweka Tanzania katika sifa nzuri ya kuwa na wananchi wenye kufuata sheria na taratibu.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeratibu Kongamano la nne la kitaifa la Watanzania wanaoishi Ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) kwa minajili ya kuwaweka pamoja watanzania hao ili kujadili kwa pamoja namna ya kutumia fursa za uwekezaji.
Kongamano hilo ni mwendelezo wa makongamano matatu ya awali yaliyofanyika mwaka 2014 na 2015 Jijini Dar es Salam na mwaka 2016 lililofanyika Mjini Zanzibar.

Lengo kuu la makongamano hayo ni kwa Serikali na wanadiaspora kukutana, kubadilishana mawazo na kuwashajihisha wanadiaspora kuwekeza nchini kwao kwa maslahi yao na kwa ustawi wa uchumi wa taifa lao.

Kongamano hili la nne la Diaspora limebebwa na dhamira ya “Uzalendo kwa Maendeleo” chini ya kauli mbiu isemayo “Mtu Kwao, Ndio Ngao”

Katika hatua nyingine washiriki wote wamepata fursa ya kujadili kwa pamoja namna bora ya kuboresha umoja huo wa watanzania waishio nje ya nchi sambamba na kutoa maoni yao kwa serikali kwa dhamira ya kuwa na Umoja na ushirikiano bora kati yao na serikali.

Pia walitembelea shamba la BIG BODY SPICE linalolima mazao mbalimbali ya
viungo ikiwemo mazao ya Pilipilimanga, Mdalasini, Kahawa, Hiliki, Vanila,
Mdoriani, Kakao, Karafuu, Tangawizi, Mrangirangi na Mkungumanga.

Baadhi Washiriki wa Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) wakifatilia Mjadala wa ufunguzi wa kongamano hilo
Mkurugenzi Mpya wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) Ndg Geofrey Mwambe akizungumza wakati wa Kongamano la nne la watanzania waishio ughaibuni linalofanyika Sea Cleaf Hotel Mjini Zanzibar
Washiriki wa Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) wakifatilia Mjadala wa ufunguzi wa kongamano hilo

Dkt Hamed Hikmany (Katikati) akiongoza mada kuhusu Ushauri wa uwekezaji kwa siku zijazo mara baada ya ufunguzi wa kongamano la nne la watanzania waishio nje ya nchi lililofanyika jana Agosti 23, 2017 Sea Cliff Hotel Mjini zanzibar

Mhe Hassan Khamis (Katikati) akiongoza mada kuhusu Jukumu la jumuiya ya Watanzania wanaoishi nje ya nchi katika uwekezaji sambamba na Diaspora na nchi yao katika maendeleo endelevu mara baada ya ufunguzi wa kongamano la nne la watanzania waishio nje ya nchi lililofanyika jana Agosti 23, 2017 Sea Cliff Hotel Mjini zanzibar

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayeshughulikia Mazingira Mhe Januari Makamba MB) akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la nne la watanzania waishio nje ya nchi lililofanyika jana Agosti 23, 2017 Sea Cliff Hotel Mjini zanzibar


Washiriki wa Kongamano la nne la watanzania waishio ughaibuni wakimsikiliza kwa makini Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayeshughulikia Mazingira Mhe Januari Makamba MB) akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo lililofanyika jana Agosti 23, 2017 Sea Cliff Hotel Mjini zanzibar

Baadhi Washiriki wa Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) wakifatilia Mjadala wa ufunguzi wa kongamano hilo
Washiriki wa Kongamano la nne la watanzania waishio ughaibuni wakifatilia kwa makini Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayeshughulikia Mazingira Mhe Januari Makamba MB) akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo lililofanyika jana Agosti 23, 2017 Sea Cliff Hotel Mjini zanzibar
Baadhi Washiriki wa Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) wakifatilia Mjadala wa ufunguzi wa kongamano hilo
Baadhi Washiriki wa Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) wakifatilia Mjadala wa ufunguzi wa kongamano hilo
Baadhi Washiriki wa Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) wakifatilia Mjadala wa ufunguzi wa kongamano hilo
Washiriki wa Kongamano la nne la watanzania waishio ughaibuni wakimsikiliza kwa makini Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayeshughulikia Mazingira Mhe Januari Makamba MB) akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo lililofanyika jana Agosti 23, 2017 Sea Cliff Hotel Mjini zanzibar.

Washiriki wa Kongamano la nne la watanzania waishio Ughaibuni (Diaspora) wakitembelea shamba la BIG BODY SPICE kujionea kilimo cha mazao ya viuongo

Washiriki wa Kongamano la nne la watanzania waishio Ughaibuni (Diaspora) wakisikiliza kwa makini maelezo kuhusu kilimo cha mazao ya viuongo mara baada ya kutembelea shamba la BIG BODY SPICE

Washiriki wa Kongamano la nne la watanzania waishio Ughaibuni (Diaspora) wakisikiliza kwa makini maelezo kuhusu kilimo cha mazao ya viuongo mara baada ya kutembelea shamba la BIG BODY SPICE


Mkwezi akionyesha umahiri wa kukwea mnazi mbele ya Washiriki wa Kongamano la nne la watanzania waishio Ughaibuni (Diaspora) walipotembelea shamba la BIG BODY SPICE



Washiriki wa Kongamano la nne la watanzania waishio Ughaibuni (Diaspora) wakisikiliza kwa makini maelezo kuhusu Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Kisasa Fumba Town Development mara baada ya kutembelea katika eneo hilo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.