ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, May 25, 2017

PICHA TUZO ZA VPL 2016/17

















ZIMBWE JR, MSUVA KICHUYA NA MEXIME WANG’AA TUZO ZA VPL 16/17.
Na Abog JEMBE FM.
Usiku wa kuamkia leo zimetolewa tuzo na zawadi kwa washindi wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara VPL katika sherehe zilizofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City.

Katika tuzo hizo, mlinzi wa kushoto wa Simba Mohamed Hussein maarufu Zimbwe Jr ameibuka mchezaji bora wa ligi kuu msimu wa 2016/17. Mabingwa wa ligi klabu ya Yanga wamekabidhiwa zawadi yao ambayo ni Tsh. Milioni 84, huku washindi wa pili,tatu na nne wakipewa zawadi zao ambao ni Simba, Azam na Kagera Sugar.

Simon Msuva na Abdulrahman Mussa pia wamekabidhiwa zawadi yao ya ufungaji bora. Tuzo ya kocha bora imechukuliwa na kocha wa Kagera Sugar Meck Mexime huku mshambuliaji wa klabu hiyo Mbaraka Yusuph akiibuka mchezaji bora chipukizi.

Golikipa bora ni Aishi Manula wa Azam huku Shiza Kichuya akitwaa tuzo ya goli bora alilofunga dhidi ya Yanga kwenye mechi ya mzunguko wa kwanza. Tuzo nyingine ni ile ya mchezaji bora wa kigeni ambayo imetua kwa kiungo wa Yanga Haruna Niyonzima, huku tuzo ya heshima ikitua kwa Kitwana Manara.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.