ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, May 26, 2017

• MWANAMUME AMUUA MKEWE KWA KUMPIGA RISASI NA YEYE MWENYEWE KUJIUA KWA KUJIPIGA RISASI WILAYANI NYAMAGANA.

MAUAJI MWANZA: Mume adaiwa kumuua mke wake kwa kumpiga risasi na yeye kujiua kwa risasi usiku wa kuamkia leo huko Mahina jijini Mwanza, polisi yathibitisha. 

Tayari Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na hii hapa taarifa kamili. BOFYA VIDEO KUIPATA TAARIFA KAMILI.

Mwanza. Mkazi wa Mahina, jijini Mwanza, aliyefahamika kwa jina moja la Max, anadaiwa kumuua mke wake, Teddy Malulu kwa kumpiga risasi usiku wa kuamkia leo. 

Baada ya kufanya mauaji hayo, Max naye anadaiwa kujiua kwa kujipiga risasi. Mpaka sasa chanzo cha mauaji hayo hakijajulikana. 

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi amethibitisha tukio hilo na kusema kuwa mwanamke anayedaiwa kuuawa na mume wake ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wavuvi Tanzania (Tafu) . 

Kamanda Msangi amesema uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea. Taarifa kamili na #video nimeiweka

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.