ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, April 19, 2017

TANZANIA KUAJIRI MADAKTARI WALIOFAA KUTUMWA KENYA.

Serikali ya Tanzania imeamua kuwaajiri madaktari waliokuwa wamepangiwa kutumwa Kenya kusaidia kupunguza uhaba wa madaktari nchini humo.

Madaktari hao walifaa kutumwa Kenya kwa mujibu wa mazungumzo kati ya ujumbe wa Serikali ya Kenya uliiongozwa na Waziri wa Afya Dkt Cleopa Mailu na Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli mwezi Machi.

Kenya ilikuwa imeomba madkati 500 na Rais Magufuli akakubali ombi hilo.

Lakini raia watano wa Kenya waliwasilisha pingamizi Mahakamani kuitaka Serikali ya nchi yao kusitisha kuajiri Madaktari kutoka Tanzania.

Mahakama ilitoa agizo la kuzuia kuajiriwa kwa madaktari hao hadi kesi iliyowasilishwa imalize kusikizwa na hadi sasa agizo hilo bado hilo. 

"Kwa kuwa hadi tarehe ya taarifa hii Mahakama nchini Kenya haijaondoa pingamizi lililofunguliwa kuhusu ajira za Madaktari wa Tanzania nchini Kenya, Rais Magufuli ameamua kuwa, Madaktari hao 258 ambao waliokuwa tayari kwenda kufanya kazi nchini Kenya waajiriwe na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara moja," taarifa kutoka kwa waziri wa afya Tanzania Ummy Mwalimu imesema.

Wizara hiyo imesema kufikia 27 Machi, jumla ya maombi takribani 496 yaliwasilishwa na kati ya hao waliokuwa wamekidhi vigezo vilivyotakiwa kwenda kufanya kazi nchini Kenya walikuwa 258.
Madaktari hao walifaa wawe tayari kusafiri kwenda nchini Kenya kati ya tarehe 6-10 Aprili, 2017 muda ambao tayari umepita.

" Serikali ya Tanzania itakuwa tayari kushughulikia upya ombi la Serikali ya Kenya kupatiwa Madaktari 500, pale ambapo hakutakuwa na vikwazo vya kupeleka Madaktari wetu nchini Kenya," amesema Bi Mwalimu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.