ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, August 20, 2016

STAND UNITED YAIKARIBISHA LIGI KUU MBAO FC KWA SARE 0-0

Kocha Mkuu wa Mbao Fc Echien Ndelgije raia wa Burundi akitoa maelekezo kwa mmoja wa wachezaji wa timu yake katika mchezo wa Ligi kuu soka Tanzania Bara kati ya Stand United ya mjini Shinyanga iliyoikaribisha Mbao Fc ya Mwanza, Hadi mwisho timu izo zilitoka sare 0-0.
 BOFYA HAPA KUPATA KILICHOJIRI.
Mchezo ukiendelea ndani ya dimba la CCM Kambarage mjini Shinyanga baina ya Stand United V mbao Fc.
Timu zote zilicheza mchezo wa kukamiana, nao mabeki wakifanya kila liwezekanalo kuweka ukuta wa nguvu kuhakikisha hakuna makosa yanayoweza kuleta madhara.
Licha ya uchanga wao Mbao Fc wamecheza soka tamu na la kuvutia lenye pasi fupifupi kiasi cha kuwastaajabisha wengi kwamba hii  ndiyo mara yake ya kwanza kutinga Ligi kuu soka Tanzania Bara.
Ndni ya dimba la CCM Kambarage.
Mshambuliaji wa Mbao Fc mbele ya ukuta wa Stand United.
Kasi ya mchezo na umakini.
Kachomoka huyo....
Kosakosa langoni mwa Stand United V Mbao Fc.
Jukwaa kuu macho kwenye kandanda.
Hata hivyo kwa mabadiliko ya Stand United, yaiyofanyika kipindi cha pili hayakuleta matokeo ya ziada.
Kocha Mkuu wa Mbao Fc Echien Ndelgije raia wa Burundi akitoa maelekezo kwa wachezaji wa timu yake katika mchezo wa Ligi kuu soka Tanzania Bara kati ya Stand United ya mjini Shinyanga iliyoikaribisha Mbao Fc ya Mwanza, Hadi mwisho timu izo zilitoka sare 0-0.
Mbao Fc.
Toka Mwanza hawa ni mashabiki wa Mbao Fc na hii ndiyo kona yao.
Utawala wa soka na hisia za wapenzi wa soka.
Hadi dakika 90 za mchezo zinamalizika.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.