Friday, January 31, 2014
ZIARA YA WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI DR.TITUS KAMANI YABAINI CHANGAMOTO ZA VITENDEA KAZI KITUO CHA UTAFITI WA SAMAKI MWANZA.
Boti ya utafiti ikiwa na Mhe. Waziri pamoja na wadau wa utafiti. |
WA G. SENGO BLOG.
MTANGAZAJI WA EATV KEN KIDAGO AFARIKI DUNIA.
NEWS:MTANGAZAJI WA TELEVISHENI YA EAST AFRICA(EATV),KEN KIDAGO AFARIKI DUNIA
Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha East Africa aliyekuwa akifanya kipindi cha 5 sports, Ken Kidago amefariki dunia.
Taarifa ambazo pia zimethibitishwa na mmoja wa wafanyakazi wa kituo hicho zinaeleza kuwa tangu jana januari 30,2014 Ken hakuonekana kazini ambapo simu zake zilikuwa zikipigwa bila majibu ikabidi uongozi wa EATV kutoa taarifa kwa jeshi la polisi nchini Tanzania,walipofika nyumbani kwake Mlalakua jijini Dar es salaam wakagonga mlango hakufungua kabidi wavunje na kuingia na kukuta amefariki.
Taarifa zinaeleza kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa sababu ya kifo chake.
Ken Kidago aliwahi kuwa mtangazaji wa Radio Ukweli ya mjini Morogoro kabla ya kwenda Arusha ambapo alirejea jijini Dar es salaam hivi karibuni na kujiunga na East Africa Television
Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha East Africa aliyekuwa akifanya kipindi cha 5 sports, Ken Kidago amefariki dunia.
Taarifa ambazo pia zimethibitishwa na mmoja wa wafanyakazi wa kituo hicho zinaeleza kuwa tangu jana januari 30,2014 Ken hakuonekana kazini ambapo simu zake zilikuwa zikipigwa bila majibu ikabidi uongozi wa EATV kutoa taarifa kwa jeshi la polisi nchini Tanzania,walipofika nyumbani kwake Mlalakua jijini Dar es salaam wakagonga mlango hakufungua kabidi wavunje na kuingia na kukuta amefariki.
Taarifa zinaeleza kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa sababu ya kifo chake.
Ken Kidago aliwahi kuwa mtangazaji wa Radio Ukweli ya mjini Morogoro kabla ya kwenda Arusha ambapo alirejea jijini Dar es salaam hivi karibuni na kujiunga na East Africa Television
KINANA, MANGULA WAWASILI MBEYA KWA MAADHIMISHO YA MIAKA 37 YA CCM.
Makamu Mwenyekiti wa CCM,Phillip Mangula akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum, Dk. Mary Mwanjelwa baada ya kuwasili leo asubuhi kwenye Ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya , tayari akwa maadhimisho ya miaka 37 ya CCM yatakayofanyika kitaifa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, jijini Mbeya Jumapili Februari 2. Kushoto ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye. |
Mangula (katikati) akiwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye (kulia) pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya, Godfrey Zambi. |
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (katikati) akizungumza na Nape (kulia) pamoja na Zambi kwenye chumba cha watu mashuhuri (VIP) alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe, Mbeya leo mchana, ttayari kwa maadhimidho hayo. |
Nape (kulia) akizungumza na Kinana pamoja na Zambi kwenye Uwanja wa Ndege wa Songwe |
Dk. Mary Mwanjelwa (kushoto) akijadiliana jambo na Makmu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi, Dogo Idd Mabrouk wakati wa mapokezi hayo.Picha na MichuziJr wa Michuzi Media Group. |
WASHINDI WA AIRTEL ‘MIMI NI BINGWA’ WAREJEA TOKA OLD TRAFFORD
Washindi wa Airtel ‘Mimi ni Bingwa’ warejea kutoka Old Trafford
WASHINDI wa awamu ya kwanza ya promosheni ya Airtel Mimi ni Bingwa jana waliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere wakitokea Old Trafford ambapo walikwenda kushuhudia mechi ya moja kwa moja ‘live’ kati ya klabu ya Manchester United na Cardiff City.
Watanzania hao wamekuwa sehemu ya washabiki wa soka waliokuwa na furaha kushuhudia klabu ya Manchester United ikishinda 2-0 dhidi ya Cardiff City, wakati mchezaji Juan Mata akiichezea timu hiyo kwa mara ya kwanza katika uwanja wa Old Trafford, hawakuweza kuficha furaha yao ya kuwa moja ya tukio hilo la kihistoria.
Akizungumza mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege, moja kati ya washindi wa tiketi ya Airtel Mimi ni Bingwa, Bw. Leonard Dickson Lyatuu kutoka Arusha, ambaye alisafiri na mke wake, alisema safari hiyo imekuwa ya manufaa sana katika maisha yao na kampuni hiyo ya simu imeweza kutekeleza yale yote waliyowaahidi washindi wa tiketi katika promosheni ya Airtel Mimi ni Bingwa.
“Ninafuraha ya kipekee kuweza kurejea nyumbani salama baada ya safari yenye mafanikio makubwa ya kwenda Old Trafford. Suala nililojifunza nikiwa Manchester ni kwamba bado Tanzania inahitaji kufanyakazi kubwa ili kuziwezesha timu zetu kuendelea katika ulimwengu wa soka. Nawashukuru Airtel kwa kunipa mimi na mke wangu nafasi ya kuwa sehemu ya historia hii na kuweza kuyatekeleza yote waliyotuahidi,” alisema.
Meneja Uhusiano wa Aitel Tanzania, Bw. Jackson Mmbando alisema wakati wa ziara ya kutembelea Old Trafford, timu ya washindi kutoka Tanzania ilionyeshwa ni jinsi gani Manchester United inawajali wachezaji wake waliostaafu, suala linalosaidia kuongeza hari katika timu na kutumia uzoefu kuiboresha timu.
“Huu ni mfano ambao wadau wetu wa michezo wanahitaji kuuiga. Tunatakiwa kuwathamini wachezaji wetu wa zamani na kutumia uzoefu wao ili kuzibadilisha timu zetu kuwa bora kimchezo kitaifa na kimataifa,” alisema.
Kwa upande wake, Andrew Muta Temwa, mshindi wa tiketi kutokea Bukoba alisema fursa ya kukutana na kocha Sir Alex Ferguson ilikuwa ni kama ndoto kwake.
“Sikutarajia kama siku moja nitakutana na Sir Alex Ferguson moja kwa moja ‘Live’. Kupitia safari hii, Airtel imeweza kuzifanya ndoto yangu kuwa kweli. Nataka kuwahakikishia washiriki wengine wa Mimi ni Bingwa waendelee kucheza ili nao wapate fursa ya kushinda pesa taslim kupitia promosheni hii ya Airtel,” alisema.
Awamu ya kwanza ilijumuisha, Bw. Leonard Dickson Lyatuu kutoka Arusha, Andrew Muta Temwa mkazi wa Bukoba, Ashraf Mohamed Adam kutoka Tanga na Salma Farid Mugheiry kutoka Dar es Salaam na wenza wao.
Airtel ilitangaza kuwa mbali na tiketi, zawadi kubwa ya shilingi milioni 50 sasa iko tayari kushindaniwa mwishoni mwa droo, ambayo kila mshiriki wa promosheni ya Airtel Mimi ni Bingwa ana nafasi ya kujishindia kwa kutuma ujumbe mfupi (SMS) wenye neno “BINGWA” kwenda namba 15656, na kujibu maswali mengi iwezekanavyo.
Washindi wa safari ya Old Trafford toka promosheni ilipoanza mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka jana ni pamoja na Msemwa George Makuzi kutoka Dar es salaam, Edwin Edmund Kajimbo kutoka Iringa, Michael Joseph Shirima kutoka Kinondoni jijini Dar es Salaam, Bw. Shaibu Rashid Dege, Mtendaji wa kijiji cha Nang’olo wilayani Kilwa – mkoani Lindi, Leonard Dickson Lyatuu kutoka Arusha, Joseph Steven Mambo kutoka Kawe jijini Dar es Salaam, Emmanuel Mahenge Jacob kutoka Njiro in Arusha, Rashid Jacob Kagombola kutoka Bukoba mkoani Kagera, Harrison Wilson Mwambogolo kutoka Kigogo jijini Dar es Salaam na Salma Farid Mughery kutoka Dar es Salaam.
MING'ARO YA SKYLIGHT BAND HUANZIA IJUMAA.
Sony Masamba a.k.a Fally Ipupa wa Bongo (kulia) akitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band huku akisindikizwa na Hashim Donode. |
Rappa Joniko Flower akifanya yake jukwaani huku Digna Mbepera na Sony Masamba wakionyesha umahiri wao wa kusebeneka. |
Muziki mzuri na watu wastarabu si pengine ni Skylight Band ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar kila siku za Ijumaa kuanzia saa usiku na kuendelea. |
Winfrida Richard akifanya yake jukwaani huku akipewa sapoti na Digna Mbepera. |
Mheshimiwa Bundala kama kawaida yake ndani ya Vest. |
Sam Mapenzi a.k.a Sukari ya warembo akililiwa asipande jukwaani na mashabiki wake. |
Kijana mtanashati kutoka kundi la Wadananda akiwa amestarehe kwenye kiti kutegeshea mrembo wa kucheza naye mdaura hapo kati..! |
Mdau Gerald Kilimo akiwa na mfanyakazi mwenzake walikuja kupunguza stress za kazi na burudani ya Skylight Band. |
Wadau wa Skylight Band na Ukodak. |
Wadau wa Skylight Band na Msanii Hashim Donode katika picha ya ukumbusho. |
Mama Kisso wakipata Ukodak na Aneth Kushaba AK 47 a.k.a Mjasiriamali mpango mzima wa kupendeza kichwani unaweza kumwona yeye...! |
Aneth Kushaba akibadilishana mawazo na Mtangazaji wa kipindi cha Mama land Benny Kinyaiya wa Clouds fm. |
JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS SASA..!!
Kuwa wa kwanza kupata Breaking News za wasanii, watu maarufu na zingine kutoka Magazeti Pendwa ya IJUMAA WIKIENDA, UWAZI, RISASI, AMANI, IJUMAA na CHAMPIONI moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa shilingi 100 tu kwa SIKU!
Kujiunga tuma GLOBAL kwenda 15778
Huduma hii ni kwa watumiaji wa Vodacom pekee. Kwa maelezo zaidi LIKE Ukurasa wetu wa Facebook hapa: http://on.fb.me/L0OSPD
Thursday, January 30, 2014
MABOMU YAFURUMUSHWA KWENYE MSIBA WA ALIYEKUWA SHEIKH WA MKOANI MARA KUWAZUIA WAFUASI WA CHADEMA WASIMFANYIE FUJO MBUNGE WA ZAMANI WA MUSOMA MJINI CCM
NA. Mwandishi wetu
Musoma.
POLISI mkoani Mara wamelazimika kutumia mabomu
kuwatawanya wafuasi wanaotajwa kuwa niwa Chama cha maendeleo na demokrasia
nchini CHADEMA waliokuwa wakimfanyia fujo aliyekuwa mbunge wa zamani wa Musoma
mjini Bw. Vedastus Manyinyi Mathayo wa CCM.
Mathayo ambaye pia alikuwa mjumbe wa NEC
inatajwa kuwa amefanyiwa vurugu hizo leo wakati alipokuwa akishiriki kuhani
msiba wa aliyekuwa Sheikhe wa Musoma Othman Magee aliyefariki dunia juzi
katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako alipelekwa kwaajili ya kupatiwa
matibabu mara baada ya kuhamishiwa toka hospitali ya Rufaa ya Bugando Mwanza
ambapo ilishindikana.
Taarifa zinasema kuwa mara baada ya
Mkutano wa hadhara wa CHADEMA kumalizika wanachama wa chama hicho wakiwa
wameambatana na Katibu Mkuu wa Chama hicho Mhe. Wilbrod Slaa pamoja na mbunge
wa Musoma mjini Mhe. Vicent Nyerere walielekea kwenye msiba kwaajili ya
kujumuika na wafiwa na wananchi wengine.
Wanachama hao walipofika kwenye msiba huo
na kumkuta mbunge wa zamani Musoma mjini Bw. Mathayo walianza kumshambulia kwa
maneno na katimaye mawe huku wengine wakiburuta pikipiki zao na kulifanya eneo
hilo kuwa na hali tete hata baadhi ya magari yakipondwa mawe kwenye eneo la
msiba huo.
Dakika chache baadaye polisi walifika
katika eneo la msiba ambalo lilikuwa si tulivu tena na kujaribu kuituliza hali
kwa njia za kidiplomasia na iliposhindikana walilazimika kurusha mabomu ya
machozi ili kupata kuwatawanya wafuasi hao.
Marehemu Sheikh Othman anatarajiwa kuzikwa
kesho mjini Musoma.
Taarifa zaidi kuwajia:- ITAENDELEA
KERO: NANI MWENYE TENDA HII MWANZA?
Ingawa ni barabara kiwango cha lami, magari yakipita ni vumbi kwa kwenda mbele . |
Taswira hailipi kabisa.... |
Wana kusanya lakini hawazoi tatizo nini? |
Taratibu wapitao wanazikanyaga taka hizo, je kwa style hii zitasalimika kurudi kwenye mitaro mvua ikinyesha? Work done zero. Au twataka tenda nyingine kuendelea kula fedha za Manispaa? |
'Tenda za kupeana hazina kukoromeana' Funika kombe mwanaharamu apite maisha yaendelee. |
VYAMA VYA NGUMI ZA KULIPWA KUUNGANA.
VYAMA VYA NGUMI ZA KULIPWA VYAUNGANA
VYAMA vya ngumi za
kulipwa nchini vimekubali kuungana na wenzao TPBO
kushiriki mkutano wa mapromota wa ngumi na mabondia wote wa Tanzania.
Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika katika ukumbi wa
vijana hall – kinondoni, siku ya jumamosi tarehe 1/2/2014
kuanzia saa nne asubuhi.
Mkutano huo ulioitishwa na TPBO chini ya udhamini wa KITWE GENERAL
TRADERS ukiwa na lengo la kuweka mikakati ya sasa na ya baadae kwa ajili ya
kuinua ngumi za hapa nchini,sanjali na kutambulikana kwa mapromota na mabondia
wenyewe kwa kutengenezewa vyeti maalum na vitambulisho, vitakavyowafanya
watambulike katika jamii ya wanamasumbwi wa hapa Tanzania na hata nje ya mipaka
ya nchi yetu,hizo ni sehemu ya mada zitakazozungumzwa.
Ibrahim
kamwe akizungumza na vyombo vya habari ,alisema ‘Mkutano huo ambao utawahusisha
mapromota wote ,pamoja na viongozi wa vyama vya ngumi za kulipwa, makocha na
mabondia wote wa ngumi za kulipwa, haijalishi wewe ni nani ili mradi ni mwalimu
wa ngumi, mratibu wa ngumi au bondia ni vema ukafika katika mkutano huo ambao
ni mara ya kwanza kufanyika katika historia ya ngumi za kulipwa
kuwakutanisha kwa pamoja waratibu, viongozi na mabondia wa nchi nzima kwa
pamoja.
Pia mkutano huo utaendana na mapromota kupewa
vyeti na kurekebisha usajili wa mabondia ambao usajili wao haujakaa
sawa.
LG YAZINDUA TV AINA YA OLED AMBAYO NIYA KWANZA KWA UBORA DUNIANI
Na mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
LG imezindua TV ya kwanza ulimwenguni aina ya OLED ambayo ndiyo imeingia katika soko ya nchini Tanzania, TV aina ya OLED inayojikunja ni mwanzo wa burudani ndani ya nyumba. Aina yake ya kujikunja ambayo inaitwa IMAX inatupa uzoefu wa hali ya juu pamoja na kuangalia kwa starehe kubwa.
TV hii mpya aina ya OLED kutoka LG ikiwa na teknolojia ya rangi nne, ambayo kwa mujibu wa kampuni inaongeza pikseli nyeupe kwa rangi nyekundu, kijani na blu kwa mtazamo bora. Itakuwa na screen nyembamba aina ya OLED ambayo ukubwa wake ni 4.3mm. Pamoja na stendi yake ambayo ina vipimo ifuatavyo 1227x799x192mm na uzito wa kilo 17.2.
TV aina ya OLED LG namba 55EA9800 inakuja na idadi ya chaguo ya kuunganisha ambayo ni HDMI port (x4), port ya kusikiliza muziki ( 3.5mm), RF, AV ( composite), port ya muziki, USB 2.0 (x2), USB 3.0 na LAN port.”
TV hii pia ina kitako ambacho ni wazi kama kioo ambacho TV huwa haionekani kama imeungana nacho na TV huonekana kama inaning’inia hewani. Pia TV hii imewezeshwa kuwa na muonekano wa spika tano kwenye kitako chenye LG 55EA9800 zenye uwezo waku toa sauti ya watti 40.
Bwana Rajesh Darji, wa Garnet Star Ltd Distributor wa LG Home Entertainment Products amesema“ Hii TV aina ya OLED inapatikana katika maduka makubwa ya LG na wakala wake.
Caption:
Picha 1. Bw. Valerian Banda ambaye ni msemaji wa Kampuni ya Garnet Star ambao ni wasambazaji wa vifaa vya LG akiongea kuelezea TV ya kwanza ulimwenguni aina ya OLED ambayo ndiyo imeingia katika soko ya nchini Tanzania.
picha 2. Mkurugeni wa Kampuni ya Garnet Star ambao ni wasambazaji wa bidhaa za LG, Tanzania, Rajesh Kumar (kulia) na Meneja Masoko wa LG, Shakti Vellu (kulia) wakisaidia kuzindua TV ya kwanza ulimwenguni aina ya OLED ambayo ndiyo imeingia katika soko ya nchini Tanzania. Uzinduzi huo ulifanyika katika duka lao lililoko Quality Center jijini Dar es Salaam.
Picha 3. Bw. Valerian Banda ambaye ni msemaji wa Kampuni ya Garnet Star ambao ni wasambazaji wa vifaa vya LG akionyesha miwani ya 3D inayotumika kuangalia kwa TV ya kwanza ulimwenguni aina ya OLED ambayo ndiyo imeingia katika soko ya nchini Tanzania.
Wednesday, January 29, 2014
MOROGORO WALIVYO SHIRIKI OPERESHENI M4C.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokreasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee wakiondoka baada ya kuhutubia mkutano wa Operesheni M4C Pamoja Daima, uliofanyika mjini Ifakara jana. |
Mwenyekiti wa Chama ch Demokrasia na Mendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akiwahutubia maelfu ya wakzi wa mji wa Mtibwa katika mkutano wa Operesheni M4C pamoja Daima jana. |
Maelefu ya wakazi wa mkji wa Ifakara, wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoja Daima, ambao ulihutubiwa na Mweneyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jana. |
Subscribe to:
Posts (Atom)