ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, March 27, 2014

SERIKALI YAIPONGEZA AIRTEL KWA KUCHANGIA MAENDELEO YA ELIMU.

Meneja biashara wa Airtel kanda ya kaskazini Brighton Majwala akimkabidhi vitabu vya sayansi kwa mkuu wa wilaya Arusha John Mongela kwa ajili ya shule ya sekondari Naura ya jijini Arusha vilivyotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya airtel chini ya mpango wake wa Shule Yetu.
Wanafunzi wa shule ya sekondari naura ya jijini Arusha wakiangalia vitabu mara baada ya kukabidhiwa vitabu hivyo na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania.
Mkuu wa wilaya ya Arusha John Mongela akimkabidhi vitabu mbalimbali mkuu wa shule ya sekondari Naura Sunday Mushobozi  vilivyotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania  katika hafla iliyofanyika shuleni hapo.
Press Release
Serikali yaipongeza Airtel kwa kuchangia maendeleo ya elimu.
Mkuu wa wilaya ya Arusha John Mongela aliwashukuru Airtel kwa msaada wa vitabu kwa shule ya sekondari ya Naura na kusema kuwa  licha ya kuwa ni jukumu la Serikali kutoa vitabu kwa shule lakini imekuwa ikizidiwa  na majukumu mengi hivyo kwa msaada huo Airtel wanapaswa kupongezwa kwa kutimiza wajibu wao kwa jamii.
Kauli hiyo imetolewa wakati Airtel ilipotoa msaada wa vitabu kwa Shule ya sekondari ya Naura mkoani Arusha chini ya mpango wake maalumu wa “shule yetu” ambapo Mkuu wa wilaya ya Arusha Bwana John Mongela alikuwa mgeni rasmi.
Bwana Mongela alisema “Vitabu ndio nyenzo ya msingi ya kupata maarifa hivyo kwa Airtel kujikita katika kusaidia jamii kupitia vitabu kwa shule za sekondari kutawawezesha wanafunzi na jamii kupata hazina kubwa ya maarifa na mbinu za kujikwamua kiuchumi kupitia vitabu hivi. Napongeza sana jitihada hizi na mpango huu ambao ni endelevu na yenye kugusa shule nyingi na jamii kubwa ya watanzania kwa ujumla”.
Meneja biashara wa Airtel kanda ya kaskazini Brightone Majwala  akizungumzia msaada huo amesema mpango huo unaolenga kutoa vifaa vya kufundishia mashuleni yaani vitabu vya hisabati, physikia, chemia na biologia  una lengo la kupunguza changamoto za uhaba wa vitabu mashuleni,   tunayofuraha  kutoa msaada wa vitabu kwa shule ya sekondari Naura kwani tunaamini wanafunzi wengi  zaidi watanufaika na kuhamasika kujiunga na kusoma masomo ya sayansi
Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo Gasper Mushobozi aliwashukuru Airtel kwa msaada huu wa vitabu vya sayansi shuleni hapa , lakini alibainisha kuwa msaada huu pia uendelezwe kwa kutuboreshea maabara ya shuleni hapo ili kuweza kupata tecknologia ya sayansi kikamilifu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.