ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, September 20, 2013

KINANA AMPA RUNGU MPINA KUWABANA MAWAZIRI.

Kutoka kushoto ni Katibu Mwenezi wa Siasa CCM Nape Mnauye (mwenye kamera),  Katibu Mkuu CCM Abdarahiman Kinana na Mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina (anaye hutubia mkutano wa ziara ya Katibu huyo wa Chama.)
HABARI KAMILI
Simiyu


KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amewataka Wabunge wa chama hicho kuwasukuma mawaziri ili waweze kutimiza wajibu wao wa kuwatumikia wananchi tofauti na ilivyo sasa ambapo wengi wao wanafanya kazi kwa mazoea.

Kinana alisema kasi ya kufuatilia utendaji kazi wa mawaziri inayofanywa na Mbunge wa Kisesa(CCM), Luhaga Mpina ni ya kuridhisha na kwamba chama hicho kinaheshimu msimamo wa mbunge huyo katika kuisimamia kikamilifu Serikali ili iweze kutimiza malengo ya kuwaletea maisha bora watanzania.

Alisema Mpina ni mbunge hodari na jasiri aliyemstari wa mbele kuwatetea wananchi na kuhoji uwajibikaji wa Serikali awapo bungeni hivyo chama hicho kitaendelea kuthamini mchango wake kwani kwa kiasi kikubwa unasaidia kuharakisha utendaji wa serikali.

"Mbunge wenu ni hodari, sisi chama tunamuheshimu, ni mchapakazi, mtetezi wenu na tunaamini mtaendelea kumchagua katika uchaguzi mkuu ujao.."alisema Kinana na kushangiliwa na maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano huo wa hadhara katika Kata ya Mwasengela jimbo la Kisesa wilayani Meatu mkoani Simiyu

Alisema matatizo mengi ya wananchi yanashindwa kutatuliwa kutokana na Mawaziri kukaa maofisini bila kufika katika maeneo husika na kwamba ufuatiliaji wa Mbunge huyo kwa kiasi kikubwa utasaidia kuwaamsha ili waweze kuchapa kazi inayotegemewa na wananchi.

Kinana alisema kazi iliyofanywa na Mpina katika utelekeza wa ilani ya CCM katika jimbo hilo ni kubwa kwani amefanikiwa kujenga miundombinu ya barabara, umeme, mawasiliano,maji, madaraja,shule za msingi na sekondari, vituo vya afya hali ambayo inakifanya chama hicho kiendelee kuaminiwa na wananchi.

Pia alisifu uwajibikaji wa Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Rosemary Kirigini katika kufuatilia kero za wananchi na kuwataka viongozi wengine kuacha kusubiri hadi madhara yatokee ndio wakimbilie kwenye maeneo hayo kutafuta suluhu.

Kwa upande wake Mpina alisema mapokezi makubwa aliyopata Katibu Mkuu huyo wa CCM ni ishara tosha kuwa Serikali imekuwa ikiwajibika kwa wananchi hasa katika jimbo hilo kwa kufanikisha kutelekezwa kwa ahadi za Rais Jakaya Kikwete alizotoa kwenye kampeni ikiwa ni pamoja na ujenzi wa daraja la Mongo-obakima ambapo wananchi walipoteza maisha kwa kuliwa na mamba na viboko pamoja na  kusombwa na maji.

Katika mkutano huo wananchi hao walimuomba Katibu Mkuu huyo wa CCM kuwatafutia suluhu ya tatizo la malisho ya mifugo hususan kwa wananchi wanaoishi kando  ya pori la akiba la Maswa kutokana na baadhi ya viongozi kuwabambikia kesi na kuwakamua fedha zao kupitia mgogoro huo wa malisho ya mifugo.

Kufuatia ombi hilo Kinana aliwaagiza Mawaziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki na Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kufika katika eneo hilo na kuutafutia ufumbuzi 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.