ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, February 14, 2013

WEZI WATATU WA ATM WAKAMATWA MWANZA

JESHI la Polisi mkoani Mwanza kwa kusaidiana na maofisa wa Benki ya NMB imewatia mbaroni watu watatu ambao wanadaiwa kuiba kiasi cha Sh700 milioni kwa nyakati tofauti.


 Watuhumiwa hao wamenaswa baada ya kuwekewa mtego na maofisa wa benki na polisi kwenye saa 6.00 usiku wa Februari 10, mwaka huu na mtuhumiwa mmoja alibambwa akichukua fedha katika ATM ya NMB kwenye Tawi la PPF Plaza Mwanza.

Baada ya kunaswa kwa mtuhumiwa huyo, alisaidia kuwaelekeza polisi walipo wenzake, ambao walikutwa katika hoteli moja jijini Mwanza wakiwa wamejipumzisha.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mwanza, Christopher Fuime alisema pia walikamata vifaa mbalimbali ambavyo walikuwa wakitumia kwa ajili ya kufanyia uhalifu huo.

Vifaa walivyokamatwa navyo
Vifaa vilivyokamatwa navyo ni kadi za bandia 194 za kuchukulia fedha katika ATM za Benki ya NMB, ambapo kati yake kadi 95 zilikuwa na namba 0225152975 zinazotumia namba ya akaunti ya 2258103695 zenye jina na picha ya mtu anayedaiwa kuwa ni mtumiaji mwenye jina la Molely L. P. Kadi nyingine 99 zilikuwa na namba 0506056317 za akaunti namba 5068000322 zikitumia jina moja la Mnuo Z. E na picha moja.
Mbali na kadi hizo pia waliweza kunasa kadi 36 za Benki za DTB, ambazo kati yake kadi 18 zilikuwa na jina moja la Kelvin G. Gratias na namba 20497883, kadi 12 zikitumia jina la John J. Paul zenye akaunti namba 2049783 huku kadi sita zikitumia jina moja la Joseph Donald akaunti namba 2049783.

Kadi nyingine tatu zenye maandishi ya Download List na nyingine ikiwa ni kadi ya Visa ya Benki ya KCB yenye namba 4183546040003827 zikitumia jina la Elikana Zacharia. Kadi nyingine zilikuwa ni tupu zisizo na maandishi wala nembo ya benki yoyote na nyingine zikiwa ni Soviet Royalty, kadi ya raia ya Urusi ikiwa na namba 000724.

Pia walikutwa na kadi ya Benki ya Amerikani yenye namba 549012345678 zilizokuwa zikitumia jina la Richard Croswell.

Walikamatwa pia wakiwa na vifaa mbalimbali vya kielektroniki ikiwamo kamera za siri tatu za kienyeji ambazo zimetengenezwa kwa kufungwa betri za simu ya mkononi na pia walikamatwa na kifaa cha kutengenezea kadi bandia (Magnetic Card reader), mikebe mitatu ya rangi za kupulizia kamera za usalama katika ATM ili wasionekane wakati wa wizi wao, ‘printer’ pamoja na kifaa cha kuchomea vifaa vya umeme.

Wizi ulivyofanyika
Wahalifu hufika katika mashine za kutolea fedha ambapo hatua ya kwanza ni kuzima kamera za usalama za eneo husika kwa kuzipulizia rangi maalumu ili kuzitia ukungu hivyo kuharibu mwonekano wake na kuruhusu wao kuingia eneo hilo bila ya kuonekana na kufanya wizi wao.
Mara baada ya kuziharibu kamera za usalama, walikuwa wakianza kwa kuweka kamera zao za siri ili kunasa namba za siri za kufungulia akaunti ambazo huzisoma katika ‘kompyuta’ na kuzinakili katika daftari lao maalumu na kisha kuchukua kadi zao bandia na kuchukua fedha.

Wizi huo wa kuchukua fedha waliufanya nyakati za usiku saa sita hadi saa tisa usiku wakati ule wa kutegea kamera zao ulifanyika muda ambao huwa na wateja wengi hasa siku za mapumziko. 

Tupe maoni yako

1 comments:

  1. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.