ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, April 28, 2012

TUNDU LISSU ASIMAMIA MZIGO WAKE 'MWENYEWE' HADI USHINDI

Mbunge wa jimbo la Singida mashariki CHADEMA),Tundu Lissu,muda mfupi baada ya mahakama kuu kutupilia mbali maombi yaliyotolewa na Shaban Selema na Pascal Halu wa CCM,kupinga matokeo yaliyompa ushindi wa ubunge. Akitoa hukumu hiyo jana, Jaji Mosses Mzuna wa Makahama Kuu Kanda ya Moshi alisema ushahidi uliotolea na upande wa walalamikaji, umeshindwa kuthibitisha kuwa, walalamikiwa walivunja au kiuka sheria, taratibu na kanuni za uchaguzi na kusababisha uchaguzi huo kutokuwa huru na wa haki, hoja zote 11 zilizoletwa na walalamikaji, zimeonyesha ushahidi wa kuhisi,kusikia na kushuku, ambao hauna uhalisia wa mambo.


Wakili Msomo mleta maombi ya Wana CCM Godfrey Wasonga akitafakari kwa hisia kali muda mfupi kabla ya kesi ya kupinga matokeo yaliyompa ubunge Tundu Lissu hayajatangazwa.


Tundu Lissu akifutwa machozi wakati wakitoka nje ya mahakama baada ya mahakama kuu kutangaza kuwa ushindi wake huo, ni halali.


Baadhi wa watu waliohudhuria kusikiliza kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi Tundu kuwa mbunge muda mfupi baada ya maamuzi hayo kutolewa ambapo kwa upande wa wao, walisema kuwa mahakama zinapaswa kuhakikisha kuwa hazibariki hoja ambazo zina mwelekeo wa kuwanyima haki wananchi viongozi wanaowataka.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.