ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, December 13, 2011

WAZAZI KUKOSA NAFASI YA KULEA WATOTO ---> CHANZO CHA WATOTO KUHARIBIKA

Grace Massawe.
Warsha ya siku tatu ya kukusanya maoni ya wadau kuhusu hali ya maisha ya mtoto anayeishi mazingira ya mijini inayofanyika jijini Mwanza imebaini kuwa, Athari nyingi zinatajwa kuwa zitaendelea kuwakumba watoto wengi nchini kutokana na wazazi wengi kukosa nafasi ya kuwalea watoto katika makuzi bora sambamba na kuwaacha bila malezi.

Akina mama wengi huondoka kwenda kwenye biashara ndogondogo na kurudi nyumbani usiku, mchana kutwa hayupo nyumbani mtoto anaamka anapaswa kwenda shule hajapata kifungua kinywa, mchana anarudi nyumbani hakuna chakula, anaamua kutinga mtaani kusaka cha kutia tumboni. Huko anakutana na changamoto nyingi zenye madhara.

Wanawarsha.
Taarifa zinakusanywa hapa ili baadae zijumuishwe kwenye mpango mkakati wa UNISEF kusaidia watoto kutoka kwenye lindi la manyanyaso ili waishi maisha stahiki.

Afisa Mtendaji kata ya Mbugani Baruan Awadhi.
Mazingira ya nyumbani yanaweza kuwa si rafiki kwa mtoto yaani hayatoi fursa kwa mtoto kujisikia kuwa yuko huru kupata huduma nzuri toka kwa wazazi ikiwemo kusikilizwa.

Sehemu ya wakusanyaji maoni kwenye warsha hiyo.

Jeshi la Polisi nalo limehusishwa.
Serikali imeweka mpango kwa kila kata kuwa na askari kwaajili ya kupata taarifa juu ya mipango yote ya uhalifu.

Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Mwanza, Stella Mbura
Wadau wajikite kwenye stadi za malezi ya watoto ili kuwanusuru watoto dhidi ya tabia chafu zitakazo isababisha nchi kupoteza uelekeo wa maisha ya baadaye.

Lengo kuu la shirika hili la hiyari linalojihusisha na harakati za kulinda na kutetea haki za watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi na magumu ni kutetea hadhi na haki ya watoto nchini Tanzania.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.