ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, December 29, 2010

HAWA NDIYO BORA KWA 2010.

Kwa kutambua mchango unaotolewa na wasanii wetu katika tasnia ya filamu mtandao huu umeguswa na kazi za wasanii hawa na kuwatambua kwa kuwatangaza, kulingana na zoezi tulilokuwa tunaliendesha la BORA ZA 2010, wadau hawa wamechaguliwa na wapenzi wa filamu hapa nchini kupitia tovuti ya www.filamucentral.co.tz kuanzia mwanzo wa mwezi december katika mtandao huu wa habari za filamu kutoka Swahiliwood.

Tunawapongeza wale wote walioshinda na kuibuka washindi katika nafasi walizoshiriki, kila aliyeingia katika mtanange huu alikuwa ni bora lakini siku ya siku tuliitaji mshindi mmoja ambaye ndiye tunamtngaza leo hii, tumefarijika sana kwa ushirikiano mlioonyesha wadau wa tasnia hii toka mwazo wa zoezi hili hadi mwisho, tunapenda kuwatambua waliotikisa mwaka 2010 na kusema Hongera.
BORA ZA 2010


1. Msanii chipukizi bora za 2010 – HANIFA DAUDI (Jenifer)
2. Muigizaji bora wa kike — YVONNE CHERRYL (Monalisa)
3. Muigizaji bora wa kiume — STEVEN KANUMBA (The Great)
4. Mwandishi bora wa mswaada – ALI YAKUTI
5. Mchekeshaji bora – ATHUMAN MUSSA ( KING MWALUBADU)
6. Filamu yenye kava bora – DANGER ZONE
7. Mtayarishaji bora wa filamu – STEVEN KANUMBA
8. Kampuni bora ya utengenezaji filamu – RJ Company
9. Msambazaji bora – Game 1st Quality
10. Muongozaji bora – VICENT KIGOSI (Ray The Greatest)

Matokeo haya ni kwa mujibu wa watembeleaji wa mtandao huu ndani na nje ya nchi.

ZAIDI TEMBELEA filamucentral.co.tz

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.