SASA MWANZA NI KILA KITU

SASA MWANZA NI KILA KITU

KARIBU KISIWA CHA RUBONDO

KARIBU KISIWA CHA RUBONDO

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, September 21, 2017

MBAO YALA SAHANI MOJA NA SIMBA.

Timu ya soka ya Simba imesimamishwa na Mbao FC kwenye uwanja wa CCM Kirumba baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 kwenye mchezo wa ligi kuu uliomalizika jioni hii.

Simba ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Shiza Kichuya dakika ya 16 kabla ya Mbao FC kusawazisha kipindi cha pili dakika ya 46 kupitia kwa Habibu Kiyombo.

Simba walishambulia kwa kasi na kufanikiwa kuongeza bao la pili dakika ya 49 kupitia kwa James Kotei. Mbao FC hawakukata tamaa na dakika ya 81 wakafanikiwa kusawazisha kupitia kwa Boniphace Maganga na kufanya mchezo huo umalizike kwa sare.

Huu ni mchezo wa kwanza raundi ya 4 ambao umewaacha Simba katika nafasi ya 2 wakiwa na alama 8 wakati Mbao FC wakisogea hadi nafasi ya 9 wakiwa na alama 4.

VIDEO:- REAL MADRID WALIVYOCHANA MIKEKA YA WANA.

 

Real Madrid vs Real Betis 0-1 - Goal & Extended Highlights - La Liga - 20/9/2017 [HD]

Wednesday, September 20, 2017

VIJANA DAR WAANZA MASOMO YA TEHAMA.

Sehemu  ya  Darasa  la  Vijana  wa  Shule za  Msingi kutoka  sehemu  mbalimbali.
 Meneja  Mradi  wa Aitel  & DTBI Computer Lab, Agape  Jengela  akizungumzia  kuhusu  mradi  huo  wa  Airtel  Fursa ambao  umenza  na  Darasa  la Vijana  wa Shule  za  Msingi  kutoka  sehemu  mbalimbali  za  jiji  la  Dar  es  Salaam, katika  fursa  hiyo  Watoto wamejifunza  kutengeneza  ROBBOT.
 Sehemu  ya  Darasa  la  Vijana  wa  Shule za  Msingi kutoka  sehemu  mbalimbali.
 Sehemu  ya  Darasa  la  Vijana  wa  Shule za  Msingi kutoka  sehemu  mbalimbali.
 Sehemu  ya  Darasa  la  Vijana  wa  Shule za  Msingi kutoka  sehemu  mbalimbali.
Sehemu  ya  Darasa  la  Vijana  wa  Shule za  Msingi kutoka  sehemu  mbalimbali.
 
Vijana Dar waanza Masomo ya Tehama
Kampuni yasimu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi)  imeanza kutoa mafunzo ya Tehama kesho katika maabara ya kompyuta iliyopo katika shule ya msingi kijitonyama na kuwawezesha vijana zaidi ya 20 waliojiandikisha kuanza kupata mafunzo hayo.

Mafunzo hayo yameanza kufatia Airtel na DTBi kutangaza kuanza kwa mafunzo hayo na kuwaalika vijana kuanzia ngazi ya shule za msingi,sekondari, vyuo vikuu na wafanya biashara kujiandikisha na kufaidika na mafunzo haya yatakayowasaidia kuvumbua application mbalimbali, kuwapatia vijana ujuzi katika mswala ya Tehama na pia kuwawezesha vijana wajasiriamali kuendesha shughuli zao za kibiashara kwa kutumia technologia za kisasa

Akiongea kuhusu kuanza kwa mafunzo hayo, Meneja Mradi wa Airtel Bi Jane Matinde alisema, Tumefurahishwa sana na muitikio mkubwa uliofanya na vijana hususani wa shule hii ya msingi ya kijitonyama na watoto kutoka maeneo mengine katika kujiandikisha na kuanza mafunzo haya. Tayari tunao jumla ya wanafunzi 20 ambapo wamejipanga kuanza kujifunza kesho kuanzia saa 9 mchana hadi saa 11 jioni.  Tunaamini hii ni fursa muhimu sana kwa vijana wetu wenye kuonyesha  dhamira yao ya kubobea katika maswala ya Tehama na komputa ya sayansi kuanza sasa wakiwa katika umri mdogo.

Bado tunapokea maombi ya kujiunga hivyo tunatoa wito kwa vijana wa sekondari , wale waliomaliza darasa la saba , wafanyabiashara kutumia vyema maabara hii yenye lengo la kuwezesha jamii  hususani vijana kuongeza ujuzi na ueledi kwenye maswala ya technologia na Tehama kwa ujumla.

Kwa upande wake Meneja wa maabara ya Airtel Fursa , Agape Jengela alisema “ Tayari tumejipanga kutoa mafunzo kwa vijana, walimu wamejipanga vyema katika kuhaikisha vijana hawa wanapata mafunzo bora. Mafunzo hayo ni pamoja na lego Robotics, program za uhuishaji kwa watoto(ziitwazo scratch) na ubunifu na uchapishaji wa“3D objects”  msingi wa kompyuta, uelewa wa kompyuta, kutengeneza program mbali mbali

Bado tunapokea maombi,   Tunato wito kwa wazazi na walezi kuwaandikisha vijana wao kwa kupitia  www.teknohama.or.tz na  www. airtelfursa.com  au kwa kutembelea maabara  iliyopo katika shule ya msingi kijitonyama

MKUU WA WILAYA YA KIBAHA ALAANI VIKALI VIONGOZI KUPIGWA RISASI,UTEKAJI WA WATOTO NA KUMTOLEA RAIS MANENO MACHAFU

Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake kuhusina na kulaani  matukio ya vitendo vya kushambuliwa  kwa viongozi kwa risasi, utakeji wa watoto sambamba na kukemea tabia ya baadhi ya watu wanaotoa maneno machafu kwa Rais Dk Joh Pombe Magufuli.
(PICHA NA VICTOR MASANGU) 

NA VICTOR MASANGU,  
GSENGO BLOG
 KIBAHA PWANI

MKUU wa   Wilaya ya Kibaha  Assumpter Mshama amelaani vikali vitendo vya matukio ya baadhi ya watu kuwavamia na kuwashambulia kwa risasi viongozi na pia hakusita kukemea tabia ya utekaji wa watoto pamoja na wale ambao wamekuwa wakimtolea maneno machafu Rais wa awamu ya Tano Dk John Pombe Magufuli kitu ambacho kinamuumiza na anachukizwa nacho.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na matukio yanayoendelea katika sehemu mbali mbali Mkuu huyo alisema kwamba anasikitishwa kuona vitendo kama hivyo vinaendelea kufanyika katika jamii ya watanzania hali ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa kwa wananchi kuishi  wakiwa katika hali ya hofu.

Mkuu huyo alisema kuwa baadhi ya watu kwa sasa  wamekuwa wakiamua kumtolea maneno machafu kiongozi wan chi bila ya kufahamu kuwa ni kinyume kabisa na sheria na taratibu za nchi kwa hivyo tabia kama hiyo haifai hata kidogo katika jamii na badala yake watanzania wanatakiwa kuwa wazalendo na nchi yao.

“Hivi karibuni ndugi waandishi mimi nachukizwa sana na kuona matukio mbali mbali yaiendelea hapa nchini, kama vile watoto kutekwa nyara, baadhi ya viongozi kupigwa risasi kwa kweli hii sio sahii kabisa hta kidogo na wengine kutoa maneno machafu kwa kiongoiz wetu wa  nchi kwa hili mimi nina laani vikali kabisa .

“Na kitu kingine napenda kuchukua fursa hii kumpa pole Mwanasheria wa Chadema Tundu Lissu kwa kuvamiwa na kushambuliwa na risasi za moto  na kumjeruhi vibaya na watu wasiojulikan, huyu Tundu Lissu ni kiongozi mkubwa na ni mtu maarufu zana hapa kwentu Tanzania lakini kitendo cha kushambuliwa na risasi sio sahii hata kidogo na mimi namwombe kwa Mungu apone na arudi kuendelea na Majukumu yake ya kuwatumbikia wananchi wa jimbo lake,”alisema.

Pia  katika hatua nyingine amebainisha kuwa serikali Wilayani Kibaha Mkoani Pwani inatarajia  kuvifutia rasmi hati viwanja zaidi ya 754 ambavyo  baadhi ya watu wamevitelekeza na kushindwa kabisa kuviendeeza kwa kipindi  cha muda mrefu hali ambayo imepelekea  kwa sasa maeneo  mengine   yamegeuka kuwa ni vichaka na  mapori makubwa ambayo yamekuwa ni kimbilio la kujifichia wahalifu pindi wanapofanya matukio ya wizi.

Tamko hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha   Assumpter Mshama wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake  kuhusiana na changamoto mbali mbali zilizopo katika suala la umiliki wa maeneo pamoja na mikakati waliyojiwekea katika kuhakikikisha maeneo ambayo hayaendelezwi yanarudishwa katika mikono ya serikali.

Mkuu huyo wa Wilaya alibainisha kwamba katika kuhakikisha anakabiliana na tatizo hilo tayari  ameshamwandikia barua Waziri wa ardhi William Lukuvi  kwa lengo la kuweza kumjulisha orodha ya watu ambao wameshindwa kabisa kuviendeleza viwanja hivyo hadi kufikia hatua ya kuwa mapori makubwa.

Nao baadhi ya wananchi Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani akiwemo Elfasi Msuya na Zakharia Cheze wakizungumza na mwandishi wa habari hizo kuhusina na tamko la Mkuu wa Wilaya kufuta umiliki wa viwanja visivyoendelezwa wamepongeza hatua hiyo ya serikali  kwani itaweza kuwapa fursa wananchi wa hali ya chini waweze kujenga makazi ya kuishi.

WILAYA ya Kibaha mkoani Pwani kwa sasa bado inakabiliwa  na changamoto ya kuwa na idadi kubwa ya viwanja ambavyo vimetelekezwa na kutoendelezwa kwa zaidi ya miaka  15 hivyo kusababisha kuwepo kwa  vichaka na mapori  makubwa ambayo yanahatarisha usalama wa wananchi kutokana na wahalifu kujificha katika maeneo hayo.

KAMANDA MUSILIMU AIPONGEZA PUMA ENERGY KWA KUWAZAWADIA WANAFUNZI WALIOCHORA PICHA BORA ZA ATHARI ZA USALAMA BARABARANI

 Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus Musilimu (kushoto), akimwangalia Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Amani, Nasri Mwema baada ya kumkabidhi tuzo ya kuwa mshindi wa kwanza kwa kuchora vizuri picha inayoelezea athari za usalama barabarani katika hafla iliyoandaliwa na Kampuni ya Uuuzaji Mafuta ya Puma Energy katika Shule ya Msingi Diamond Dar es Salaam leo. Mashindano hayo yanadhaminiwa na Puma Energy Tanzania. Kulia ni Msajiri wa Hazina, Oswald Mashindano na Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Phillipe Corsaletti. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
 Mwanafunzi Nasri Mwema  akipokea tuzo kutoka kwa Msajiri wa Hazina , Oswald Mashindano (kulia),.Anayeshuhudia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Puma, Phillipe Corsaletti.
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Puma, Phillipe Corsaletti akipongezana na  Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus Musilimu 
  Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus Musilimu  na viongozi wengine wakishiriki kuteua picha bora tatu zilizochorwa na wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi Mkoa wa Dar es Salaam.

Mwanafunzi George Jonas wa Shule ya Msingi Upendo akikabidhiwa begi na madaftari yenye alama za usalama barabarani baada ya kuwa mshindi wa tatu  katika mashindano hayo
 Mshindi wa pili wa shindano la uchoraji wa picha za kuonesha athari za usalama barabarani, Rehema Mzimbili  wa Shule ya Msingi Buza, Temeke, Dar es Salaam, akipokea


 Mshindi wa Kwanza Nasri Mwema akiwa katika picha ya pamoja na viongozi baada ya kukabidhiwa zawadi ambapo pia Shule yake ya Amani ilizawadiwa sh. mil. 2.

 Kamanda Musilimu akionesha picha iliyoshinda katika mashindano hayo
Washindi wote watatu wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi pa walimu wao

KATIBU MTENDAJI BODI YA FILAMU AWATAKA WATANZANIA KUJIANDAA TAMASHA LA JAMAFEST.

Binagi Media Group
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Tanzania Bi.Joyce Fisso amewataka watanzania kujiandaa na kutumia vyema fursa ya kuwa wenyeji wa Tamasha la Utamaduni na Sanaa Afrika Mashariki (JAMAFEST) litakalofanyika nchini mwaka 2019.

Akizungumza na BMG hii leo, Bi.Fissoo ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la JAMAFEST 2017 lililomalizika Kampala nchini Uganda, amesema tamasha hilo linatoa fursa kubwa kwa watanzania kuonyesha ngoma na bidhaa mbalimbali za kiutamaduni na hivyo kukuza soko lao la ndani na nje ya nchi.

Aidha Bi.Fissoo amefurahishwa kwa namna watanzania walivyoshiriki vyema kwenye tamasha la mwaka huu nchini Uganda na kubainisha kwamba walitia fora kwenye maonyesho ya tamasha hilo yaliyofanyika kwenye viwanja vya Kokolo.

Katika kilele cha Tamasha la Utamaduni na Sanaa Afrika Mashariki JAMAFEST mwaka 2017 nchini Uganda, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Tanzania, Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe alipokea bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kama ishara ya Tanzania kuwa mwenyeji wa tamasha hilo ambalo kwa mara ya kwanza liliasisiwa nchini Rwanda mwaka 2013.

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi Tamasha la JAMAFEST Bi.Joyce Fisso (mwenye bendera) akijiandaa kupongea cheti cha pongezi kutoka kwa Waziri wa Wizara ya Afrika Mashariki ya Uganda Mhe.Ali Kivejinja kwenye kilele cha Tamasha la Utamaduni na Sanaa Afrika Mashariki JAMAFEST lililofanyika Kampala nchini Uganda Septemba 14,2017.
Naibu Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Balozi Elibariki Maleko (wa pili kulia) akipokea cheti cha pongezi kutoka kwa Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bi.Joyce Fissoo kwenye kilele cha Tamasha la JAMAFEST ambapo Tanzania ilishiriki vyema kwenye tamasha hilo lililofikia tamati Septemba 14,2017 nchini Uganda.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini, Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe alipokea bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kama ishara ya Tanzania kuwa mwenyeji wa Tamasha la Utamaduni na Sanaa Afrika Mashariki JAMAFEST mwaka 2019 ambapo kwa mara ya kwanza tamasha hilo liliasisiwa mwaka 2013 nchini Rwanda.